Habari

Papa Francis apingwa na kutetewa baada ya kusema kuzimu haipo

Na mwandishi wetu,

Kwa mujibu wa gazeti la Italian News Paper Papa Francis ameingia kwenye gumzo nzito alhamisi iliyopita baada ya kunukuliwa akisema kuwa kuzimu haipo.

Eugenio Scalfari, mwanzilishi mwenza wa gazeti la Repubblica, alichapisha mazungumzo aliyofanya na Papa Francis hivi karibuni.

Katika makala hiyo, Scalfari alisema alimuuliza Papa Francis ikiwa “Roho zenye dhambi” huadhibiwa baada ya kufa.

“Hawana adhabu! wale ambao wanatubu wanapata msamaha wa Mungu na kwenda miongoni mwa roho zilizokubaliwa na Mungu, lakini wale ambao hawakutubu, hawawezi kusamehewa na hutoweka .. Hakuna kuzimu, kuna upotevu wa roho za dhambi, “Scalfari alinukuu kauli za Papa Francis.

Maelezo hayo yalizua utata na mijadala mikali katika ulimwengu wa Kikristo, huku watu wengi wakimshtaki Papa kwa kuwa kinyume na maandiko.

Ofisi ya habari ya Vatican imedai kwamba taarifa za Papa si za nukuu moja kwa moja, bali hayo ni mawazo ya mwandishi.

“Kilichoripotiwa na mwandishi katika makala ya leo ni matokeo ya mawazo yake, ambapo maneno yaliyotamkwa na Papa hayakunukuliwa. Hakuna kifungu cha nukuu kilichotajwa hapo na kuhesabiwa kama sehemu inayotuaminisha kuwa ni maneno ya Baba Mtakatifu, “Vatican ilisema katika taarifa hiyo. Japo kwa siku kadhaa za nyuma mwandishi Eugenio Scalfari, alikiri ukweli kwamba hana rekodi au kuandika maelezo hayo ya Papa Francis wakati wa mahojiano.

Licha ya mjadala mkali juu kupinga maneno ya Papa Francis, Katekisimu ya Kikatoliki bado inakubali na kuunga mkono kuwepo kwa kuzimu.

Kifungu cha 1035 cha Katekisimu kinasema: “Mafundisho ya Kanisa yanathibitisha kuwepo kwa Kuzimu na milele yake. Mara baada ya kufa, roho za wale wanaokufa katika hali ya dhambi huingia kuzimu, ambapo watakabiliwa na adhabu za kuzimu, moto wa milele. Adhabu kuu ya kuzimu ni kutengwa milele na Mungu, Mtu peke yake ndiye anayeweza kumiliki maisha na furaha tangu kuumbwa kwake na kuishi. ”

Jack Graham, mchungaji wa Kanisa la kisabato (Prestonwood Baptist Church), anasema kuzimu ni sababu ya Wakristo kusherehekea Jumapili ya Ufufuo.

“Hakuna papa, kuhani, mchungaji au mtu anayeweza kuhamisha kuzimu kwa kukataa ukweli wake.” kuzimu ni ukweli halisi na usioepukika tunapaswa kukabiliana nayo. Kwa kweli, kuzimu ndiyo sababu ya miaka 2,000 iliyopita siku ya Ijumaa kama leo Yesu alisulubiwa. Yesu alikufa kifo ambacho sisi wote tulikuwa tunastahili na amelipa adhabu ya milele ya kuzimu ambayo tulipaswa kulipa, “alisema. “Hatukatai kuzimu: kuzimu ni kweli, lakini Yesu ni shujaa.”

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Tony Richie Feat. Limoblaze – Mirror

Next post

Mchungaji aliyejaribu kumfufua mfu akamatwa Msumbiji