Habari

Papa Francis kutembelea Latvia, Lithuania na Estonia mwaka 2018.

Na Mwandishi Wetu;

Papa Francis amepanga kutembelea nchi ya Latvia, Lithuania na Estonia mwaka ujao, wakati mataifa hayo matatu yakisherehekea maadhimisho ya miaka 100 ya umoja wao.

Janis Siksnis, mshauri wa rais wa Latvia, alithibitisha kupitia umoja wa vyombo vya habari alhamisi iliyopita, akisema hakuna maelezo mengine yaliyopatikana mpaka sasa kuhusiana na ujio wake nchini humo.

Msemaji wa Rais wa Lithuania Dalia Grybauskaite, Daiva Ulbinaite, mapema ameliambia shirika la habari la Baltic kwamba ziara hiyo ilipangwa kwa msimu wa mwaka 2018, na mpaka sasa bado wanasubiri serikali Vatican itoe tamko juu ya tarehe kamili ya ziara hiyo inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Papa kutembelea nchi za umoja wa Baltic ambapo mnamo Septemba 1993, Papa John Paul II aliweza kutembelea nchi hizo akianzia nchi ya Lithuania ambayo ina jumuiya kubwa ya kikatoliki katika jumuiya ya nchi za Baltics ambapo ina zaidi ya asilimia 75 ya wakazi ambao ni sawa zaidi ya watu milioni tatu ambao wote ni wakatoliki.

Mataifa matatu ya Baltic yalitangaza uhuru wao kutoka kwenye mikono ya Urusi mwaka wa 1918 lakini yaliingizwa katika umoja wa Sovieti mwaka wa 1940 na ikawa sehemu yake mpaka 1991.

Mpaka sasa Papa Francis ana ziara moja ambayo tayari imeshathibitishwa kwa mwaka 2018, ziara hiyo itaihusisha nchi ya Chile na Peru kuanzia Januari 15 – 22, na anatarajiwa pia kutembelea kisiwa cha Ireland mwezi Agosti kushiriki katika mkutano wa familia duniani(World Meeting of Families).

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio Music: Yz Manamba - Nasubiri

Next post

Selena Gomez kwa machozi aweka wazi ushuhuda wake na kusema 'Mimi ni Mtoto wa Mungu'