Habari

Padri mwengine auawa nchini DRC

Na mwandishi wetu,

Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri aliyefahamika kwa jina la Étienne Nsengiyumva alikuwa akikomunisha waumini na ndipo mtu mmoja mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.

Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.

Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Farlon Lyte – My Advantage

Next post

Audio: Seya - Be-You-Tiful