Connect with us

Official Audio Music: Rhoda Itenya – Funguka

Muziki

Official Audio Music: Rhoda Itenya – Funguka

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu! kwa utukufu wa Mungu leo nimekuletea wimbo mpya unaoitwa Funguka kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Rhoda Itenya au unaweza kumwita Riama Itenya, wimbo ukiwa umefanyika ndani ya studio za Exodus chini ya mikono ya Prodyuza Kameta.

Funguka ni wimbo uliobeba ujumbe wa matumaini kwetu sisi wana wa Mungu ambao kwa namna tofauti tofauti tumekuwa tunapitia majaribu ya aina mbalimbali ndani ya dunia hii ambayo imejaa kila aina ya dhambi lakini kupitia mtumishi wa Mungu Rhoda Itenya leo anatukumbusha kuwa Yesu yupo na kupitia roho wake mtakatifu anatenda maajabu katika maisha yetu, hivyo hatupaswi kuishi kwa kujutia dhambi zetu bali kwa kumtegemea Yesu na kumweleza vile shetani anavyokutesa na yeye atahakikisha anazisafisha dhambi zako na kuwa mpya na kujazwa baraka.

Hakika ni wimbo mzuri uliojaa maneno ya kuitia moyo sana, kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana siku ya leo

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Rhoda Itenya Kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 360 866
Facebook: Riama Itenya
Instagram: @riamaitenya

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top