Music

Audio Music: A.O Chuks – Honestly Speaking

Kutoka nchini nigeria! leo kupitia tovuti yako pendwa nimekuwekea wimbo wa sifa uitwao Honestly Speaking (Nasema Kwa uaminifu) ukiwa ni wimbo wa shukrani unaotukumbusha mambo ambayo Mungu ametutendea kwa ajili yetu.

Akizungumza kwa msisitizo mtumishi wa Mungu A.O Chucks amesema kuwa: ”Nimesukumwa kuandika wimbo huu baada ya kukumbuka mambo ambayo Mungu amefanya kwa ajili yangu. amenipenda na kunipokea nikiwa sina chochote na kunipelekea mahali ambapo ni pa juu sana. Nina kila sababu ya kusema kwa uaminifu kutoa shukrani zangu kutoka ndani ya moyo wangu na kumhamasisha msikilizaji wa nyimbo hii kumwamini Mungu na kwamba ikiwa amefanya hivi kwa ajili yangu basi anaweza kufanya hivyo pia kwa mtu mwingine.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina amini utakubariki sana. Karibu!!

 

Download Audio

Social Media:

Facebook: Chukwudifu Agbagwu
Instagram: @a.o.chuks
Twitter: @achuksy
YouTube: Chukwudifu Agbagwu

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Je Unafahamu Mungu Alikuumba kwa Kusudi Gani?

Next post

Audio Music: Bishop Abrah Soja Feat Kibonge wa Yesu - Liwalo na Liwe