Connect with us

Nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi oktoba 2017, hizi hapa.

Muziki

Nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi oktoba 2017, hizi hapa.

Shalom mwana wa Mungu leo kwa mara nyingine tena nimekusogezea nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri zaidi mwezi oktoba 2017.

Katika mwezi wa kumi tumeona mfululizo wa kuachiwa kwa nyimbo nyingi nzuri kutoka kwa waimbaji mbalimbali walio ndani na nje ya afrika mashariki na kushuhudia baadhi ya waimbaji kadhaa kama vile Jessica Bm Honore, Benny William, Gilbert Noah, Pamsam na wengine wengi ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa na mwitikio mkubwa zaidi kutoka kwa wasikilizaji walioweza kutembelea tovuti ya gospomedia.com na vyombo vingine vya habari ikiwemo radio na blogs zingine.

Hizi hapa ni orodha rasmi ya nyimbo 10 bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa oktoba 2017.

1. Jessica Bm – Furaha Yangu

2. Benny William – Wa Ajabu

3. Gilbert Noah – Usiniache

4. Pamsam – Asante

5. Ivan Mosha – Siku Hazigandi

6. Rhoda Itenya – Ni Neema

7. Kenny Polz – Anafanya

8. Felista Gabriel Kiduu – Ninalindwa na Nguvu za Mungu

9. Dr. Tumaini Msowoya – Hakuna Matata

10. Ajuwae Onesmo – Wengi Wamejisahau

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa nzuri na bora kiufundi(Music Quality) lakini pia kufanikiwa kuwagusa na kuwabariki watu wengi zaidi na hili ndilo kusudi kuu katika kulitangaza neno la Mungu. Barikiwa!

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top