Connect with us

Njia 5 za kupunguza tumbo (kitambi) kirahisi

Jinsi ya kupunguza tumbo kirahisi

Dondoo

Njia 5 za kupunguza tumbo (kitambi) kirahisi

WANAUME NA WANAWAKE wengi wanatamani kuwa na matumbo madogo, lakini wengi hushindwa kufikia ndoto hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uzazi na kupenda chakula. Dondoo hii itakusaidia njia rahisi ya kupunguza tumbo.

1. UANGALIFU KATIKA KULA
Epuka chakula chenye wanga, mafuta mengi na sukari. Badala yake unaweza kula matunda na mboga za majani. Vile vile samaki wa baharini si wabaya kwani hawana mafuta mengi.

2. NAMNA YA KULA
Usiache kula kwani jambo hilo litakunyima nguvu, unatakiwa kula milo mitatu mpaka minne lakini kwa kiasi kidogo. Unatakiwa kukaa zaidi ya saa tatu kabla ya kula mlo mwingine.

3. MAZOEZI YA KAWAIDA
Si lazima ufanye mazoezi makali kwa ajili ya kupunguza tumbo. Unaweza kufanya zoezi la kutembea badala ya kupanda basi, kama hufiki mbali sana. Kama unaweza kuogelea, unaweza kufanya hivyo mara kwa mara, hiyo pia itakusaidia.

4. ZOEZI MAALUM
Kama unaweza kufanya zoezi la kulala chali na kukaa, ‘abs exercise’ unaweza kufanya kwa dakika chache kila siku. Hiyo itasaidia kukomaza misuli ya tumbo hivyo tumbo kutokulegea.

5. KUNYWA MAJI
Maji yanasaidia mmeng’enyo wa chakula, hilo husaidia mtu kuwa na afya njema. Kwa kuwa mtu akiwa katika hatua za awali za kupunguza tumbo husikia njaa mara kwa mara, ni bora anywe maji badala ya kula.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

TRENDING

To Top