Connect with us

NIGERIA: Pasta Adai Watu Maskini ni Wale Simu Zao Huita Wakiwa Kanisani

Pasta Adai Watu Maskini ni Wale Simu Zao Huita Wakiwa Kanisani

Top Stories

NIGERIA: Pasta Adai Watu Maskini ni Wale Simu Zao Huita Wakiwa Kanisani

Kiongozi wa Kanisa la Salvation Ministries, Pasta David Ibiyeomie, amewaelezea wale ambao simu zao hupigwa wakiwa kanisani kama watu maskini.

Pasta huyo alitoa matamshi hayo akihubiri katika ibada Jumapili, Novemba 21, akiongeza kuwa matajiri hawana tabia hiyo. Daily Trust inaripoti kwamba alisema mtu tajiri huwa makini sana wakati wa ibada kusikiliza mahubiri ya kumfanya kuwa mtu bora.

”Lakini watu maskini huwasha kwa sababu wanataka arifa; ambayo ni ishara ya umaskini. Huwezi kamwe kuona mtu tajiri akiwasha simu yake kanisani, atasema, “Nataka kusikia kitu ambacho kitasaidia kuboresha maisha yangu,” alisema. Alidai kuwa kinyume na mtu maskini, atawasha simu kanisani sababu ana matumaini kuwa kuna mtu atamtumia pesa.

Chanzo: TUKO

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top