NEWZ:Edna Kuja kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Gospo? - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

NEWZ:Edna Kuja kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Gospo?

Audio

NEWZ:Edna Kuja kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Gospo?

Pengine unaweza ukawa umeanza kumsikia kwenye wimbo wake uliobeba album yake mpya,AMENIFUTA MACHOZI,kwa taarifa yako Edna kuja hii ni album yake ya pili ukiacha ile ya PUMZIKO LA ROHO.Edna Kuja alianza kupenda muziki akiwa msichana mdogo kabisa,alikuwa akipiga ngoma na kuimba kanisani na amekua hivyo mpaka akajikuta tayari yupo kwenye tasnia ya Muziki wa Injili Tanzania.
Tofauti na waimbaji wengi ,malengo makuu ya Edna katika Uimbaji wake yamekuwa ni kuleta uhai katika muziki wa Injili,kutumiwa na Mungu kama chombo kugusa maisha ya watu ambao Mungu amewakusudia.
Edna,ambaye sasa ni mama wa watoto wa wawili kwa mume mmoja anahisi kama ndio ameanza rasmi huduma kwa kuweka nguvu zake zote kwenye album yake mpya ya Amenifuta Machozi ukiachana na ile ya kwanza ambayo aliifanya akiwa chuo hivyo kukosa uhuru zaidi wa kutumika ipasavyo.
Licha ya sasa kuwa mwimbaji binafsi akipata sapoti toka kwa familia yake hasa mume wake,Edna aliwahi kuwa katika kundi la Youth Gospel Entertainment,kundi lililokuwa likihubiri Injili kwa njia ya muziki wa kizazi kipya ndani yake kukiwa na waimbaji kama Rungu la Yesu,DP,Against Devil na wengineo toka mwaka2006 hadi mwaka 2008 alipohamishiwa kikazi mkoani Tanga.
Ukiacha yeye mwenyewe kuwa mwanadada anayesifika kwa viwango vya juu katika kazi zake Edna anavutiwa na waimbaji wengi ambao wanafanya kazi zao kwa viwango wakiongozwa na waimbaji Miriam Lukindo na Angel bernad kwa kuwataja wachache.
Edna anatarajia kuzindua album yake ya pili,Amenifuta machozi tarehe 3/5/2015 katika ukumbi wa Ubungo Plaza na kutakuwa hakuna kiingilio ili kuwawezesha watu wote kuhudhuria(GospoMuziki tutakuwa tunakupa kila kitachokua kinajili),pia ameachia wimbo wake wa Umenifuta machozi ambao ndio umebeba jina la album.
Sikiliza wimbo wa Amenifuta machozi kutoka kwa Edna Kuja.

Continue Reading
You may also like...

More in Audio

To Top