Habari

NEWZ:DOXAZ MUSIC MANAGEMENT,FUTURE YA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.

Muziki wa Injili ni tasnia kubwa sana duniani pengine naweza sema ni kubwa kuliko zote.Napata ujasiri wa kusema hivi kutokana na ukweli kwamba kanisa ndio chimbuko kuu la waimbaji wengi zaidi duniani kote na ukizingatia kuwa asili ya muziki ni mbinguni ambapo walioko huko wanamsifu Bwana kila kukicha ukiachana na Lucifer aliyehasi cheo alichopewa na Mungu cha kuwa malaika mkuu wa sifa.
Ukiachana na hayo yote historia za waimbaji wengi sana hata wasio wa “gospo” zinaonyesha kuwa walianza kuimba kanisani na badae kuingia kwenye muziki wa “secular” kwa lengo la kupata maslahi zaidi na mengineyo ,Japo siamini kwamba muziki wa kidunia unaleta maslahi zaidi kuliko muziki wa Injili ukichukilia mfano wa nchi zilizopigia hatua na kuuchukulia muziki wa Injili kama kazi na biashara nyeti bila kusahau lengo la kutoa huduma hivyo kufanya sanaa hiyo kuwapatia fedha nyingi huku wakibariki mioyo ya watu.
Kwa hapa nyumbani kwetu Tanzania hali ya muziki wa Injili ni tata kidogo,pamoja na kuwa ni tasnia yenye waimbaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu ukiongeza na upako lakini bado umekuwa ukisuasua kupelekea waimbaji kupata maslahi madogo au kutopata kabisa wakiamini ni kazi ya Bwana lolote na liwe na kuleta mgongano wa maswali kama ,muziki wa injili ni kazi,biashara au huduma?swali ambalo tutalijadili siku za mbeleni.
Tuachane na hayo tuongee kidogo yanayohusu kichwa cha habari chetu kuhusu Doxaz Music Management ambayo makao yake makuu yako Arusha ikiwa inahusika na swala zima la kuwasimamia wasanii wa “gospo” kuwa “Brand” na kuwa “promote” na pia swala nzima la kusamamia uandaaji wa matukio mbalimbali.
Nilipata nafasi ya kuongea na Rais wa Doxaz Music Management,Bw.Sakafu Godsave ambaye maneno yake ndio yamenipa mshawasha wa kuandika utangulizi kama ulivyousoma hapo juu.Kihistoria Bw.Sakafu anasema yeye amekuwa mwimbaji toka mtoto kipaji ambacho anaamini amerithi kwa baba na babu yake na mpaka sasa amefanikiwa kutoa album mbili ambayo moja ameishaitoa na anaiuza mkononi na nyingine ya pili ambayo anataraji kuizindua tarehe 24/05/2015 katika ukumbi wa Golden Tower 6th Floor,posta huku akishirikiana na mke wake mtarajiwa Bi.Angel Bernad ambapo mradi huo wameuita “IT’S ON” wakizindua DVD mbili kwa wakati mmoja.
Jambo lililonivutia zaidi kutoka kwa Bw.Sakafu ni hatua aliyoamua kuchukua kutoka kuwa mwimbaji tu wa kawaida na kuwa mtu ambaye anasaidia waimbaji wengine kutimiza ndoto zao.Godsave anasema kuwa aliona waimbaji wengi wanashindwa kufika malengo ya kile kitu ambacho Mungu ameweka ndani yao kwa sababu wengi walioshika hatamu hawana moyo wa kuwasaidia ila wana agenda zao binafsi mojawapo ikiwa ni kujipatia pesa tu kupitia wao,pia na kutokana kuwa haridhishwi na ubora wa kazi za wasanii wa “gospo” ambao wengi wao hawana uwezo wa kufanya kazi katika kiwango kikubwa hivyo yeye kama mtu anaependa muziki na anapenda kuona watu wanakua ilibidi aingilie kati kuokoa jazi na kuanzisha Doxaz.
Godsave ameweka wazi kuwa Doxaz inatumia fursa ya maendeleo ya kiteknolojia kuhakikisa waimbaji walio chini yake wanafanya kazi zenye hadhi za kimataifa na kutumia fursa hiyo kujitangaza pia bila kusahau kuwafundisha waimbaji umuhimu wa “self Branding” kama msanii na “Self discipline katika huduma ili waweze kufanikiwa zaidi. Pia Bw.Godsave aliongeza kuwa mipango ipo mingi ikiwa pamoja na kuchukua wasanii wapya ambapo muda ukifika watatoa taarifa kwenye vyombo vya habari ,mpaka sasa Doxaz inamsimamia mwimbaji Angel Bernad ambaye ana mkataba wa kudumu ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kum “rebrand” msanii huyo,bila shaka ukiangalia video ya Need you to reign ya Angel imeziacha mbali sana kwa ubora kazi ambazo alizitangulia kuzifanya hapo mwanzo na sasa wanakuja na full DVD ya msanii huyo,pia Doxaz inafanya kazi na MoS kwa mkataba.
Japo ambalo nawapongeza Doxaz ni kutambua kuwa muziki ni sanaa,kazi,huduma,taaluma na kuwa unahitaji kuwa “Branded” na kufanywa kwa ubora mkubwa sana japo ambalo wasanii wengi wa “Gospo” hawalitilii maanani wakidai kuwa bora punda afe ila mzigo ufike,yani kufikisha ujumbe bila kujali ubora wa kazi zao,hakika kama Doxaz watafanyia kazi hayo waliyoyatambua basi wataufikisha mbali saana muziki wa injili.
unaweza kuwasiliana na uongozi wa Doxaz kupitia doxamusic7@gmail.com au +255759444488.

Advertisements
Previous post

VIDEO: UNIGUSE - The Twins,Jacob & Joshua Mvena.

Next post

NEWZ: WAIMBAJI WA GOSPO KUMUIMBIA KIKWETE.