NEWZ: SABABU TANO KWANINI HUTAKIWI KUKOSA KWENYE USIKU WA VIPAJI WA YESU OKOA MITAA,IJUMAA HII. - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

NEWZ: SABABU TANO KWANINI HUTAKIWI KUKOSA KWENYE USIKU WA VIPAJI WA YESU OKOA MITAA,IJUMAA HII.

Habari

NEWZ: SABABU TANO KWANINI HUTAKIWI KUKOSA KWENYE USIKU WA VIPAJI WA YESU OKOA MITAA,IJUMAA HII.

Jeshi la Yesu Okoa Mitaa ,YOM Project Tanzania wakishirikiana na Mchungaji Bonventure Katembo wa kanisa la TAG Deliverance Church ,Tabata Chama wanakuletea Tamasha la Usiku wa Vipaji litakalofanyika usiku wa tarehe 8/5/2015 kuanzia saa tatu na nusu usiku hadi alfajiri.
Tamasha hilo ambalo litafanyika kanisani hapo litapambwa na waimbaji kutoka Yesu Okoa mitaa ambao ni Rungu la Yesu,SirMbezi,EkaInjili,Magele winner,Brian Mwimba,Amani Shabani,Ray 2 Jay,Esta Mbuguni,Mic Gower,Batazal MoreFire na George Maige pia waimbaji wengine kama Neema Lyimo,Neema Chavala,Joshua ndaki,Josephine Kato bila kusahau kwaya ambazo ni Born Winners,Elgibo choir,Deliverance Choir na Adonai Choir.
Leo nilipata nafasi ya kuongea na mwenyekiti wa Yesu Okoa Mitaa,Rungu la Yesu ambao ndio watu wanahodhi tamasha hilo na alinipa sababu tano kwanini hutakiwi kukosa tamasha hilo,hizi hapa…
1.kwanza kabisa tamasha hili halibagui mtu yeyote,sio la dini Fulani,kabila Fulani,rika Fulani,rangi Fulani na kutakuwa hakuna kiingilio kwa hiyo hakuna sababu ya mtu yeyote kukosa.
2.Pili utapata kusikiliza aina zote za muziki kuanzia Worship,HipHop,R&B,Sebene na kila aina ya muziki ambao utakwepo siku hiyo ili mradi uwe una mtukuza Mungu.
3.kwa yeyote mwenye kipaji atapata nafasi ya kuonyesha kipaji chake,cha kufanya awasiliane mapema na uongozi kupitia namba 0712 348 032
4.Tamasha litafanyika ijumaa usiku hadi asubuhi,kutakuwa na muda mwingi wa kujiachia mbele za Bwana pia kushuhudia mambo mengi zaidi.
5.Mchungaji Katembo atakufundisha jinsi ya kugundua kipaji chako.
Mwisho Rungu la Yesu anasema kuwa tamasha hili ni kwa ajili ya kuwapa jukwaa waimbaji wa muziki wa injili kuonyesha vipaji vyao na kumsifu Mungu kwa ukuu zaidi.

More in Habari

To Top