Newz: Je Kuna Bifu kati ya hawa mastaa wa Gospo wa Kenya?Ona mmojawapo alichopost Instagram. - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Newz: Je Kuna Bifu kati ya hawa mastaa wa Gospo wa Kenya?Ona mmojawapo alichopost Instagram.

Audio

Newz: Je Kuna Bifu kati ya hawa mastaa wa Gospo wa Kenya?Ona mmojawapo alichopost Instagram.

Msanii maarufu wa gospo Kenya, Bahati ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Lover ,leo amezua gumzo katika mtandao wa instagram baada ya kupost picha ya mkali mwenzie wa Gospo nchini Kenya,Willy Paul na kumtupia tuhuma kadhaa.
Bahati ameandika barua hiyo ya wazi kwa Willy akidai ameshindwa kumwambia moja kwa moja kwa kile alichodai kuwa nyota huyo hapokei simu zake na humjibu kwa jeuri pale anapomtumia ujumbe mfupi wa maneno.
“Kaka kumbuka umekuja kwenye muziki miaka minne kabla yangu ila kwanini unapenda kunifanya nijisikie kama tuko kwenye mashindano,je kila ninapotoa wimbo kuna ulazima wa wewe kutaka kukimbilia au kujiandaa kutoa na wewe wa kwako?,umewaambia watu wengi kwamba wimbo wako wa vigelegele umeuachia tu ili kufanya watu wasipokee vizuri wimbo wangu wa Lover”
Hayo ni baadhi ya maneno machache(yametafsiriwa) ambayo Bahati amemtuhumu Willy Paul na kumwambia kuwa yeye hafanyi muziki tu bali anafikisha ujumbe aliopewa hata Mungu angetumia kitu kingine mbali na muziki bado angefanya huku akishangazwa kuwa inakuaje wanafanyiana hivo ikiwa wote wameokoka.
Sio hivyo bali Bahati ameenda mbali na kumtuhumu kuwa Willy hutuma wapelelezi ili kujua yeye anafanya nini ili wampiku na kulalamika kuwa tayari Willy ameshamuibia nyimbo kadhaa.
b1
b2
b3
b4

Continue Reading
You may also like...

More in Audio

To Top