Habari

NEWZ: GOSPEL RAPPER NOVIC ATANGAZA KUACHIA NGOMA MPYA “NIMEKIRI” NDANI YA CAMPUS NIGHT YA MOSHI.

Rapper,hit maker wa Ukweli Halisi Novic Daniel baada ya kimya cha kitambo sasa amefunguka kuwa ngoma mpya iko karibuni kukamilika na ataichia soon kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,lakini kubwa ya yote Novic ameweka wazi kuwa kwa mara ya kwanza atawazawadia mashabiki wake watakaohudhuria tamasha la Campus night litakalofanyika ndani ya Moshi tarehe 16 Januari 2015 kwenye viwanja vya CCM Mkoa,ambapo Novic pamoja na rappers wengine kama King remmy na Uncle Ema wamepata shavu la kushambulia jukwaa siku hiyo.
Katika Single hiyo ambayo ni ya pili katika mixtape yake ya GOSPEL RAP,Novic ameibua vipaji vipya kabisa ndani ya muziki wa HipHop akiwepo rapper wa kike Julieth na rappers wengine kama F One,WaKristo,G Tano pamoja na yeye mwenyewe ambapo wote ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Arusha.
Kazi kwenu mashabiki kaeni mkao wa kula.

Advertisements
Previous post

NEWZ:RAPPER DOUGLAS KYUNGAI KUACHIA TUSEMEZANE FEBRUARY.

Next post

Gospo Audio Song: Ebeneza - MoreFire FT. Joyce Ombeni & Teophil