Habari

NEWZ: Goodluck George,Modo aliyejitoa kwenye Gospo.

Goodluck akiwa kazini,RAK Studios.

Goodluck akiwa kazini,RAK Studios.

GoodLuck George akiwa katika moja ya kazi yake.

GoodLuck George akiwa katika moja ya kazi yake.

Kijana mahiri katika tasnia ya filamu na modeling,GoodLuck George ameihabarisha GospoMuziki.Com kuwa sasa ameamua kujitoa zaidi kufanya kazi na wanamuziki wa injili,hii ikiwemo pamoja na kucheza drama kwenye video ,kutokea kwenye matangazo na maonesho ya modeling kwenye matukio mbalimbali.
Goodluck ambaye kwa sasa anafanya kazi kama model kwenye studio za RAK amesema amefikia uamuzi baada ya kuona kuwa vitu kama hivi ni muhimu lakini mara nyingi havitiliwi mkazo kwenye tasnia ya muziki wa injili hasa hapa kwetu Tanzania.
“Unajua Modeling na Video vicxing ni kazi za kitaalamu kabisa,na sisi tunafanya kitaalamu na kwa weledi,lakini wanamuziki wengi huchukulia kuwa mtu yeyote anaweza kufanya, kitu ambacho kinapunguza umakini na ubora wa kazi,na ndio maana mimi nmejitoa katika hili kuhakikisha kuwa tunafanya kitaalamu hili kufikisha tasnia hii hatua za juu zaidi,naamini kila mmoja akicheza katika nafasi yake tutafanikiwa” alisema Goodluck katika mahojiano na GospoMuziki.com na kwa kuanzia ameshaanza mazungumzo na rapper maarufu wa Gospo HipHop nchini Eka Injili ambapo atatokea kwenye tangazo la wimbo wake mpya ambao anatarajia kuutoa hivi karibuni.
GoodLuck George anapatika kwenye mitandao ya kijamii kwa jina hilo,kwa mtu yeyote anayetaka kufanya nae kazi anaweza kumcheki kupitia 0716 16 00 07.

Advertisements
Previous post

Throw Back/Old skul:Unaikumbuka hii ya Munisi Kumlilia Malebo?..Kama umeimiss icheki hapa.

Next post

New Gospo Video: Wingu la utukufu - Faustine John.