Mafundisho

NENO LA LEO: KWANINI YESU ALITESEKA NA KUFA? SOMA HAPA

Katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka jumapili ya leo tarehe 27.03.2016 GospoMedia imekuletea makala fupi ya utafakari kuhusu mateso, kufa na kufufuka kwa Mwana wa Mungu Yesu kristo ambaye kupitia matukio haya yaliyotokea miaka mingi iliyopita hadi leo bado watu wote duniani tunakumbuka vile matendo hayo yalivyo na nguvu juu ya kujenga Imani za wakristo wengi duniani.

Mwaka wa 33 W.K., Yesu Mnazareti aliuawa. Alishtakiwa kwa uwongo kuwa mchochezi, akapigwa kikatili, na kutundikwa mtini. Alikufa kwa maumivu makali sana. Lakini Mungu alimfufua, na siku 40 baadaye, Yesu akapaa kwenda mbinguni.

christ

Simulizi hilo la pekee linatoka katika Injili nne za Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, ambazo hujulikana kama Agano Jipya. Je, kweli mambo hayo yalitukia? Hilo ni swali muhimu sana. Ikiwa mambo hayo hayakutukia, imani ya Kikristo ni bure na tumaini la uzima wa milele katika Paradiso ni ndoto tu. 1 Wakorintho 15:14 14  Lakini ikiwa Kristo hakufufuliwa, hakika kuhubiri kwetu ni bure, na imani yetu ni bure. Kwa upande mwingine, ikiwa mambo hayo yalitukia, basi kuna tumaini zuri ambalo unaweza kupata. Kwa hiyo, masimulizi ya Injili ni ya kweli au hadithi tu?

HABARI ZA UHAKIKA

Tofauti na hekaya zilizobuniwa, masimulizi ya Injili ni sahihi na yanaeleza mambo hususa. Kwa mfano, masimulizi hayo yamejaa majina ya maeneo halisi ambayo yanaweza kutembelewa leo. Yanataja kuhusu watu halisi, ambao wanahistoria wamethibitisha kwamba waliishi.—Luka 3:1, 2, 23 “3  Katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa gavana wa Yudea, na Herode alipokuwa mtawala wa wilaya ya Galilaya, lakini Filipo ndugu yake alikuwa mtawala wa wilaya wa nchi ya Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mtawala wa wilaya ya Abilene,  katika siku za mkuu wa makuhani Anasi na za Kayafa, tangazo la Mungu likamjia Yohana mwana wa Zekaria nyikani “.

 Yesu anatajwa na waandishi wa karne ya kwanza na ya pili. Kifo chake kinachofafanuliwa katika Injili kinapatana na jinsi Waroma walivyokuwa wakiwaua wahalifu. Pia, matukio yanaelezwa kwa unyoofu na kwa undani hata makosa ya baadhi ya wanafunzi wa Yesu. Mathayo 26:56; Luka 22:24-26; Yohana 18:10, 11 “56  Lakini yote haya yametukia ili maandiko ya manabii yatimizwe.” Ndipo wanafunzi wote wakamwacha na kukimbia. Mambo yote hayo yanaonyesha wazi kwamba waandishi wa Injili walikuwa wanyoofu na walisema mambo kwa usahihi kumhusu Yesu.

UFUFUO WA YESU

tomb

Ingawa watu wengi hukubali kwamba Yesu aliishi na kufa, baadhi wana mashaka na ufufuo wake. Hata mitume wake hawakuamini waliposikia kwa mara ya kwanza kwamba amefufuliwa. Luka 24:11 “11  Hata hivyo, maneno hayo yalionekana kama upuuzi kwao nao wakawa hawawaamini wanawake hao” Hata hivyo, waliamini kwamba Yesu amefufuliwa walipomwona katika pindi tofauti-tofauti. Hata katika kisa kimoja, watu 500 walimwona Yesu.— Wakorintho 15:6  Baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa wakati mmoja, ambao walio wengi kati yao wapo mpaka sasa, lakini wengine wamelala usingizi katika kifo.”

Bila kuogopa kukamatwa na kuuawa, wanafunzi wa Yesu waliwatangazia watu wote ufufuo wa Yesu kwa ujasiri—hata wale waliomuua. Matendo 4:1-3, 10, 19, 20; 5:27-32 19  “Lakini Petro na Yohana wakajibu wakawaambia: “Kama ni jambo la uadilifu mbele za macho ya Mungu kuwasikiliza ninyi badala ya Mungu, hukumuni ninyi wenyewe. 20  Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema juu ya mambo ambayo tumeyaona na kuyasikia.”Je, wanafunzi hao wote wangekuwa na ujasiri kama wasingekuwa na uhakika kwamba Yesu amefufuliwa? Kwa kweli, ufufuo wa Yesu umewachochea watu wengi ulimwenguni wavutiwe na Ukristo sasa na wakati uliopita.

Masimulizi ya Injili ya kifo na ufufuo wa Yesu ni sahihi. Ukiyasoma kwa makini utapata uhakika kwamba matukio hayo ni ya kweli. Usadikisho wako utaimarishwa zaidi ukielewa kwa nini mambo hayo yalitukia.

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

JITAMBUE: HIVI UNAJUA KUWA WEWE NDIO MPANGO MZIMA? SOMA HAPA KUJUA

Next post

ZAWADI YA PASAKA KUTOKA KWA ZEPHANIAH BAHHE - MTETEZI WANGU YU HAI. DOWNLOAD HAPA.