Audio

Audio: Nehemia Kindole – Wema na Fadhili

Kutoka mjini Bagamoyo leo kwa mara ya kwanza nimekuletea wimbo uitwao Wema na Fadhili kutoka kwa muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Nehemia Kindole. Muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Canaan chini ya mikono ya prodyuza Joshua Ndaki.

Akizungumzia ujumbe ulio katika wimbo huu muimbaji Nehemia Kindole amesema:-

”Ninaitwa Nehemia Kindole ni muimbaji mpya kabisa katika uimbaji wa muziki wa Injili hapa Tanzania namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kukamilisha wimbo huu ambao nina imani kuwa utakwenda kuwagusa watu wa Mungu kupitia kazi hii. Wimbo huu unaitwa Wema na Fadhili, ukielezea wema wa Mungu wetu ambao unatufuata kila iitwapo leo. Ujumbe wa wimbo huu umetoka kwenye kitabu cha zaburi 23 Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.” – Nehemia Kindole

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu nina imani utabarikiwa sana!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Nehemia Kindole kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 117 943
Facebook: Nehemia Kindole Email:  kindolenehemia@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Sinach – In Love With You

Next post

Audio: Judith Mbilinyi - Jina la Yesu