Video

Music Video | Audio: Neema & Paul – Nitetee

Kutoka jijini Dar es salaam, leo kwa utukufu wa Mungu nimekuwekea video iitwayo Nitetee kutoka kwa kundi jipya la waimbaji katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania hawa si wengine bali ni Neema na Paul ambao kwa pamoja wamekusudia kufikisha ujumbe huu kwako mwana wa Mungu hasa wewe uliyekosa tumaini na amani katika maisha yako na leo kupitia wimbo huu utapokea tumaini jipya litakalokupa nguvu ya kusonga mbele zaidi.

”Tumeachia wimbo huu kwa kusudi la kuleta neno la matumaini kwa watu walioingiwa na kusumbuliwa na roho ya kukata tamaa kwa yale waliyopitia na wanayoendelea kupitia hivyo kupitia wimbo huu tunawakumbusha na kuwasisitiza kuwa Mungu yupo kamwe hakuwahi kumwacha mwenye haki akiteketea ni lazima atamtetea tu, hivyo tunakusihi sana mwana wa Mungu usikate tamaa endelea kuamini katika Yesu Kristo naye atafanya jambo kuu katika maisha yako.” – walisema Neema na Paul.

Video ya wimbo huu imeongozwa na director Debro Gabriel kutoka studio za Eagle View na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Van K chini ya mikono ya prodyuza Michael.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video na kupakua wimbo huu ambao nina imani utakubariki na kukuinua. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na kundi la waimbaji hawa kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 673 433 183
Facebook: Neema Alex | Paul Lameck
Instagram: @neema_alex | @paul_lameck
Youtube: Neema Aleex

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio Music: Massin - Side

Next post

Music Audio: Neema Mudosa - Hawawezi