Music

Audio: Neema Ng’asha – Naamini

Kutoka jijini Mwanza, leo nimekuletea wimbo mzuri wa kuabudu uitwao Naamini kutoka kwa Neema Ng’asha akiwa ni moja kati ya waimbaji mahiri na wanaofanya vizuri zaidi jijini Mwanza kwasasa, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Exodus chini ya mikono ya prodyuza Gilbert Noah.

”NAAMINI ni wimbo unaotukumbusha kuwa Mungu sikuzote yuko pamoja nasi, kuna wakati tunapitia mambo magumu ya kuumiza na kukatisha tamaa na tunajiona kama tuko peke yetu, lakini jambo la msingi ni kujua kwamba hatuko peke yetu, majaribu huja ili kuimarisha imani zetu, MUNGU siku zote yuko pamoja nasi nyakati zote, na ushindi ni lazima kwetu, hivyo tusikate tamaa.” – Alisema Neema Ng’asha.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri utakaoifanya akili yako imtafakari Mungu katika viwango vya juu na vya tofauti kabisa, Bwana Yesu asifiwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Blog: www.neemangasha.blogspot.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari, muziki wa Injili na Matangazo. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio: Shasha Solo - We ni kila kitu kwangu

Next post

Video | Audio: Angel Benard - Utukumbuke