Connect with us

Neema Ng’asha Kuachia Albamu Mbili Kwenye Tamasha kubwa la Muziki wa Injili, Tar 10 Disemba 2017.

Matukio

Neema Ng’asha Kuachia Albamu Mbili Kwenye Tamasha kubwa la Muziki wa Injili, Tar 10 Disemba 2017.

Kutoka jijini Mwanza, Mwimbaji wa nyimbo za  Injili Tanzania Neema Ng’asha ametangaza rasmi ujio wa tamasha lake kubwa la uzinduzi wa album zake mbili mpya moja ikijulikana kwa jina la Usilie Tena itakayokuwa kwenye mfumo wa Audio CD na ile nyingine iitwayo Tunae Bwana itakayokuwa kwenye mfumo wa Video DVD.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Neema Ng’asha alikuwa na haya ya kusema; ”Napenda kuwafahamisha watu wote kutoka ndani na nje ya Tanzania kuwa tarehe 10 disemba mwaka huu nitafanya Tamasha kubwa la muziki wa Injili litakalohusisha uzinduzi wa albamu zangu mbili mpya katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwakweli namshukuru sana Mungu kwa hatua hii niliyoifikia kwakuwa haikua rahisi kutimiza kusudi hili huku nikiwa nimetingwa na changamoto nyingi sana lakini bado mpaka sasa naamini kuwa kuna sehemu iliyobaki ambayo Mungu atakwenda kunipigania ili Injili ya Bwana isonge mbele, Album zangu zitakazo zinduliwa siku hiyo ni pamoja na TUNAE BWANA (DVD) na USILIE TENA( Audio CD) na nathibitisha kuwa waimbaji wengi binafsi kutoka jijii Mwanza na kwaya mbalimbali zimethibitisha kuwepo katika tamasha la uzinduzi wa albamu hizi ambazo ninaamini zitakwenda kuwa ushuhuda na nuru ya matumaini kwa watu wengine, hivyo nawaomba wakazi wa jijini Mwanza, kanda ya ziwa na mikoa yote ya jirani kwa ujumla wasikose kufika uwanjani kuanzia saa nane mchana nakuendelea, Naamini Mungu atakwenda kuwahudumia watu wake kwa njia ya tofauti na ya kipekee sana lakini pia naomba mje kunitia moyo kwa kununua albamu zangu.” – Alimalizia Neema Ng’asha.

Mwimbaji neema Ng’asha kwasasa anatamba na video yake iitwayo Matendo Yako ikiwa imeongozwa na director Jay Menge kutoka studio ya Calm Media na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Jungle Records chini ya mikono ya producer Sam Mboya.

Kama bado hujapata nafasi kutazama na kupakua wimbo huu kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kupakua wimbo huu ambao kwa hakika utakubarikiwa na kipaji cha mwimbaji huyu. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu uzinduzi wa album zake, kupata nakala na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Blog: neemangasha.blogspot.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top