Connect with us

Video: Neema Ng’asha – Kheri Krismasi na Mwaka Mpya

Audio

Video: Neema Ng’asha – Kheri Krismasi na Mwaka Mpya

Kwa mara nyingine tena mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza maarufu kama Neema Ng’asha ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Kheri ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Video hii imeongozwa na director IP Magera kutoka studio za Smart Vision International.

“Huu ni wimbo ambao nimeutoa kama zawadi kwa watu wote ambao wanaomwamini Kristo na kuwatia moyo kwa kuwatakia kheri ya mwaka mpya, Yawezekana kabisa kuwa mwaka huu wa 2018 mipango na juhudi zako zimeshindwa kuonyesha matokeo mazuri lakini hiyo sio sababu ya kukukatisha tamaa unapaswa kuongea na Mungu akupe ujasiri wa kusonga mbele zaidi ya hapo ulipoishia, Amen” – alisema Neema Ng’asha.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki kwa namna ya kipekee, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Youtube: Neema Ng’asha

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top