Audio: Neema Ng'asha - Akisema Ndio - Gospo Media
Connect with us

Audio: Neema Ng’asha – Akisema Ndio

Audio

Audio: Neema Ng’asha – Akisema Ndio

Baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake uitwao Naamini kwa mara nyingine tena kutoka jijini Mwanza, Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng’asha ameachia wimbo wake mpya uitwao Akisema Ndio, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Apex Music chini mikono ya prodyuza Ben William.

“Ujumbe wa wimbo huu ni kutukumbusha kuwa Mungu ndiye msemaji wa mwisho katika maisha yetu, AKISEMA AMESEMA kwa jina la YESU litatimia, Kuna wakati adui anatusemesha maneno ya kutukatisha tamaa kuwa haiwezekani lakini tunatakiwa kusimama katika imani kuwa inawezekana,  Kutoka katika 2 Wakoritho 1:20
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. – Alisema Neema Ng’asha.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri na tunaamini kuwa utakubariki kila wakati utakapokuwa unausikiliza, Bwana Yesu asifiwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Youtube: Neema Ng’asha.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top