Music

Music Audio: Neema Mudosa – Hawawezi

Shalom mwana wa Mungu leo kwa mara nyingine nimekusogezea wimbo mzuri sana uitwao Hawawezi kutoka kwa mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akifahamika kwa jina la Neema Mudosa. wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Mpo Africa chini ya mikono ya Goodluck Gozbert.

Hawawezi ni wimbo mzuri uliobeba ujumbe wenye kusudi la kukupa nguvu ya kuamini katika ushindi ndani ya Yesu, tunajua kuwa hali ya dunia ya leo imejaa misongo na majaribu ya kila aina ambayo mengi yanasabishwa na binadamu wenyewe kiasi ambacho unarudi nyuma na kumwacha Mungu lakini leo kupitia wimbo huu Neema Mudosa anakutia moyo na kukuhimiza kukiri ushindi juu ya watu wanaotaka uanguke na kuwa mbali na Mungu..

Tambua kuwa upendo na mipango ya Mungu juu ya maisha yako haiwezi kuzuiwa wala kubadilishwa na binadamu yoyote kwakuwa yeye pekee ndiye mwenye mamlaka juu yetu na vyote vilivyopo duniani na mbinguni.. hivyo amini Hawawezi kubadilisha mpango wa Mungu, kusudi la Mungu juu yako.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani utaufurahia, utakubariki na kukuinua. Karibu!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Neema Mudosa kupitia
Simu/WhatsApp: +255654 782 575
Facebook: Neema Guillaine Mudosa
Instagram: @neemamudosa

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Audio: Neema & Paul - Nitetee

Next post

Music Video | Audio: Promise Ndonge - Vitumbua na Mchicha