Connect with us

Video: Neema K – Wewe ni Mungu

Muziki

Video: Neema K – Wewe ni Mungu

Shalom mwana wa Mungu leo kutoka jijini Nairobi, nimekuwekea video ya wimbo wa kuabudu uitwao Wewe ni Mungu kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za injili kutoka kwenye label ya Crosslife Movement Production iliyopo nchini Kenya.

Mwimbaji huyu anafahamika kwa jina la Neema K na video ya wimbo huu imeongozwa na director mahiri anayefahamika kwa jina la  Bakari Ousman kutoka studio za Crosslife Movement na wimbo ukiwa umeandaliwa na prodyuza Paul Kinyari.

Wewe ni Mungu ni wimbo wa kuabudu uliobeba sifa na utukufu kwa Mungu na kupitia uwezo wa sauti ya mwimbaji Neema K ni hakika utapata kubarikiwa na kuinuliwa kwa viwango vingine vya tofauti ambavyo vitakufanya umtafakari Mungu kwa upya, kumsifu na kumtukuza katika roho na kweli.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nzuri ikiwa imebeba baraka za Mungu naamini itakwenda kukubariki na kukuinua kwa kadri utakapokuwa unazidi kuusikiliza wimbo huu… Wewe ni Mungu!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Neema K kupitia:
Facebook: Neema K
Instagram: @officialneemak
Youtube: Neema K

Advertisement

TRENDING

To Top