Video | Audio: Natasha Lisimo - Mfariji - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Natasha Lisimo – Mfariji

Audio

Video | Audio: Natasha Lisimo – Mfariji

Baada kuachia video ya wimbo wake uitwao Ufunguo akiwa amemshirikisha mwimbaji mkongwe Bahati Bukuku,  Kwa mara nyingine tena kutoka jijini Dar es salaam tumekusogezea video mpya ya wimbo uitwao Mfariji kutoka kwa mwimbaji anayefahamika kwa jina la Natasha Lisimo.

Video hii imeongozwa na director Fahim na George kutoka studio za Rehoboth Pictures, Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za JCI Records.

“Huu ni wimbo wa maombi naamini kila wakati unapokuwa unaangalia wimbo huu utayachukua maneno haya na kuyafanya yako na kumpelekea Mungu, Maana yeye ni MFARIJI wa kweli, YESU KRISTO AKUTANE NA HITAJI LA MOYO WAKO.” – alisema Natasha Lisimo

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema, Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Natasha Lisimo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 655 770 007
Facebook: Natasha Tresor Lisimo
Instagram: @natashalisimo
Youtube: Natasha Lisimo

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top