Connect with us

‘Nataka Kufanya Mapenzi ya Mungu’ – Harry Connick Jr. Akiri Imani Yake.

Habari

‘Nataka Kufanya Mapenzi ya Mungu’ – Harry Connick Jr. Akiri Imani Yake.

Mwimbaji, mwigizaji, na muongozaji wa kipindi cha Televisheni Harry Connick Jr., anasema Mungu ndiye msingi wa kila kitu anachofanya katika maisha yake.

“Kama nitaulizwa ni mambo gani matatu niyataka maisha yangu nitajibu ninataka kufanya mapenzi ya Mungu, nataka kufanya mapenzi ya Mungu, nataka kufanya mapenzi ya Mungu,” alimwambia mtangazaji Matthew Faraci wakati wa mahojiano kwenye Channel ya Dove.

Wakati wengine wanaweza kuona kufanya mapenzi ya Mungu kama ni kitu cha kuudhi au kutokufurahisha, Connick anaamini kufanya mapenzi ya Mungu kunampa ubunifu zaidi na nguvu.

“Ninataka tu kufanya kile ninachopaswa kufanya, nikiamini kwamba huo ndio msingi ambao kila kitu kinajengwa, kufanya mapenzi ya Mungu inanifanya kuwa kama mtoto na kunaniwezesha kuwa na hisia na ubunifu zaidi.”

Connick ni moja kati ya wasanii 60 bora wa kiume wenye mauzo makubwa zaidi kwenye muziki wa Jazz na albamu zake nyingi zimekuwa na mafanikio makubwa kupitia chati kubwa za muziki nchini marekani.  Umaarufu wake ulionekana zaidi na jina lake kukua haraka katika sekta ya muziki toka miaka ya 90, na baada ya hapo aligeukia sekta ya filamu na televisheni, na kwenda mbali zaidi.

Licha ya umaarufu wake, Connick hakuwa na aibu juu ya imani yake kwa Mungu. Anatumia kipindi chake cha majadiliano kiitwaco “Harry Talk show” kuelezea maoni yake mengi juu ya Mungu.

“Mimi huwa sihubiri kwenye kipindi changu cha majadiliano na maonyesho(talk show) kwa sababu mimi si mhubiri na sijihusishi na mambo ya siasa kwa sababu mimi ni mburudishaji na nataka tu kuwa na kipindi kitakachowafurahisha mashabiki zangu,” alisema.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top