Video | Audio: Nardo Turid - Hakika - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Nardo Turid – Hakika

Video

Video | Audio: Nardo Turid – Hakika

Kutoka jijini Nairobi Kenya leo nimekusogezea video ya wimbo uitwao HAKIKA kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Nardo Turid, video ya wimbo huu imeongozwa na director Sammy D kutoka studio Trued Pictures na muziki ukiwa umetayarishwa na mikono ya prodyuza Jorham kutoka nchini Uganda.

”Kwa majina naitwa Nardo Turid, ni mzaliwa wa DR Congo, South Kivu, Bukavu, lakini kwasasa naishi Nairobi Kenya nikiwa nafanya biashara na masomo, mimi ni mzaliwa wa pili katika familia ya watoto 4, na bado wazazi wangu wako hai, I thank God!. Napenda sana kuimba, hasa nyimbo za kusifu nakuabudu, na kilichonifanya nitunge wimbo huu “Hakika” ni kwasababu ulifika wakati ambao nilianza kujutia upendo wa Mungu katika Maisha yangu, nilikuwa naona Mungu anapendelea wengine lakini mimi namuomba na yeye anakuwa kimya, Nikasema moyoni mwangu labda wengine ni watakatifu, Mimi mwenye dhambi, lakini mwishoe akanionesha vile vitu sikua naona kwa macho ya mwili, things which prove that he really loves me, he cares about me, vitu pesa haiwezi kununua, na ndipo hapo akanipa wimbo huu “HAKIKA”. – Alisema mwimbaji Nardo

Ni hakika utabarikiwa na kuinuliwa kiroho kila utakapokuwa unaitazama video hii na kusikiliza wimbo huu ambao ni HAKIKA Yesu atakuweka huru kweli kabisa kwa kuwa anakupenda, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Nardo Turid kupitia:
Simu/WhatsApp: +254 715 467791
Facebook: Nardo Turid
Instagram: @nardoturidofficial
Youtube: Nardo Turid

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

To Top