Habari

Nani Atashinda katika vipengele vya muziki wa Injili ‘BORA Awards 2017’?

Orodha ya wateule wa tuzo za BORA 2017 imetangazwa rasmi na baadhi ya wasanii maarufu wa muziki injili kutoka nchini nigeria wamefanikiwa kutangazwa rasmi. Ni vipengele viwili tu vya muziki wa Injili katika toleo la mwaka huu ndio vimetangazwa kwenye tuzo hizo, ikiwa ni pamoja na ‘Best Male Gospel Gospel’ na ‘Best Female Gospel Artiste’.

Hii ndio orodha kamili ya wasanii ambao watashiriki kushinda tuzo hizo mwaka huu.

Best Male Gospel Artiste

FRANK EDWARDS
BUCHI
STEVE CROWN
NATHANIEL BASSEY
SAMMIE OKPOSO
JOE PRAIZE

Best Female Gospel Artiste

SINACH
ONOS
NIKKI LAOYE
ADA
CHIOMA JESUS
JOAN PAUL

Sherehe ya tuzo hizo zimepangwa kufanyika Jumamosi, Oktoba 28, 2017, katika ukumbi wa Eko Hotel na Suites, Victoria Island, mjini Lagos.

BORA ni kifupi cha ‘Best of the Republic Awards ‘ zikisimamiwa na Kampuni ya Credible Forte (ikiwa ni mwanachama wa Kampuni ya Inkline), iliyopo nchini Nigeria.

Pamoja kuwa sherehe hizo zitakuwa ni zenye kufana sana, sherehe ya tuzo za BORA pia huleta pamoja watu wenye vipaji mbalimbali wakiwemo wasanii, pamoja watu mbalimbali kutoka kwenye sekta tofauti tofauti kama vile Burudani, Serikali(sekta za uma) na Sekta Binafsi. Tuzo zinawasilishwa kwa mafanikio bora ya mwaka katika vipengele tofauti tofauti, pamoja na mafanikio ya muda mrefu kutoka kwa watu mbalimbali watakaotajwa kuwa washindi siku hiyo, ambapo tuzo yenye picha za EAGLE zitatolewa kwa wapokeaji(Washindi).

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Walter Chilambo kuachia albam yake hivi karibuni

Next post

Namba Moja ya Walter Chilambo yapokelewa vizuri