Nafikiri kanisa linatakiwa kuwakaribisha wenye dhambi - Snoop Dogg - Gospo Media
Connect with us

Nafikiri kanisa linatakiwa kuwakaribisha wenye dhambi – Snoop Dogg

Habari

Nafikiri kanisa linatakiwa kuwakaribisha wenye dhambi – Snoop Dogg

Rapa Snoop Dogg amejibu hoja za wakosoaji wanaohoji kuhusu kuingia kwake katika tasnia ya muziki wa injili.

Rapa huyo mkongwe katika kiwanda cha hip-hop nchini marekani, ambaye jina lake kamini ni Calvin Broadus mwezi Februari 2018 aliachia rasmi albamu yake ya Injili, iitwayo ‘Bible of Love’ aliyowashirikisha waimbaji wakubwa wa nyimbo za Injili kama vile Tye Tribbett, Fred Hammond, na B. Slade (ambaye zamani alijulikana kama Tonex).

Gazeti moja liliripoti kuwa nyota hao wa nyimbo za injili walijitolea na kuungana na Snoop ili kuandaa albamu hiyo.

Wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye tuzo za Stellar Gospel Music Awards, Snoop aliweza kuelezea mabadiliko yake ya maisha na muziki kutoka katika muziki wa kidunia(Secular Music) hadi muziki wa injili.

“Siku zote kuna kitu kilikuwa ndani yangu tangu nilipoingia katika sekta ya muziki, siku zote nilikuwa na ushawishi wa kufanya muziki wa injili,” Snoop alisema.

Na alipoulizwa kile anachokifikiria kuhusu watu ambao hawakufurahishwa na maamuzi yake ya kufanya muziki wa injili, Snoop alieleza moja kwa moja juu ya hamasa yake katika albamu yake mpya na mapingamizi hayo yanaweza kufanya nini juu ya maoni yao.

“Huu si mradi unaoendeshwa na fedha – ni mradi unaoendeshwa na roho,” alisema.

Aliendelea, “Ikiwa kanisa limejaa watakatifu tu haitakuwa sahihi. Kwa hivyo, ukimpata mtu anayejaribu kutafuta njia ya kurudi nyumbani, jambo la asili tunalotakiwa kufanya ni kumkabiribisha kwa unyenyekevu, fungua mikono yako na useme “Ndugu, tumekupokea kama ulivyo, tunajua umekuwa ukifanya makosa na unataka kupata haki na tunataka kukusaidia kupata haki. “Hatuwezi kukutupia mawe wakati unapojaribu kupata haki na kurudi kwenye nyumba ya kanisa na hayo ndiyo mambo yanayowakimbiza watu na kuwaweka nje ya kanisa.

Kisha akageukia kamera, akiwaambia watazamaji na akasema: “Vipi kuhusu wewe? Umeangalia hali yako? Je, unakwenda mbinguni? Kwanini unanihukumu? Umefanya kiasi gani kwa Bwana?”

Siku 5 zilizopita, rapa huyo alishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard nchini Marekani.

“Kwa mapungufu yote yanayoonekana katika ulimwenguni wa sasa, nadhani ni wakati mzuri wa kufanya kitu chanya ili kuwaleta watu pamoja,” alisema wakati akizungumza katika tamasha la Essence Festival Machi 27, 2018.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top