Habari

Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Marekani Raia wa Tanzania Happy Kweyamba Auchia Rasmi Wimbo Wake Mpya.

Happy kweyamba ni mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Marekani katika mji wa Dallas Texas na ni mzaliwa wa mkoani mbeya Tanzania na sasa amejiwekea maisha yake huko ambapo pia anafanya kazi na huduma zake za muziki wa Injili na wakati mwingine hata akiwa huku nchini Tanzania kwa mapumziko.

Akizungumza na gospomedia mubashara toka mjini Dallas Texas, Marekani Happy amesema kwamba ameuachia rasmi wimbo wake wa Our Father kwa mfumo wa Video ambapo wimbo huo ameufanyia huko nchini Marekani na upo tayari kwa mitandao na unachezwa kwenye vituo vya Tv hapa nchini Tanzania na huko Marekani.

Wimbo huu nimeuimba katika lugha zote mbili kwa maana ya kiswahili na kiingereza na hii nimefanya ili wote wasikie wa huku nilipo ugenini na nyumbani pia waelewe nini nimeimba, pia video hii nimeifanyia huku Texas lakini audio nimefanyia nyumbani Tanzania ni wimbo mzuri na audio nzuri ambayo mtu akiusikiliza kwa mara ya kwanza atainuliwa kiroho na hatakuwa kama mwanzo namshauri msomaji aweze kuutazama wimbo wangu na kuusikiliza naamini atanijulisha namna Mungu atakavyombadilisha , Our Father maana yake ni Baba Yetu”. Alisema muimbaji Happy Kweyamba.

Happy Kweyamba yupo tayari kwa mialiko mbalimbali ya kihuduma na anapatikana kwa mawasiliano yafuatayo:
Facebook: Happie Kweyamba
Instagram: Happy Kweyamba/happie_amos
Youtube: Happy Kweyamba.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia.

Advertisements
Previous post

Download & Download Music Audio: Beatrice Kitauli Feat Rose Muhando-Wajue

Next post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Baraka Jimmie - Jina