Mwimbaji Tumaini Msowoya ashinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Elimu - Gospo Media
Connect with us

Mwimbaji Tumaini Msowoya ashinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Elimu

Habari

Mwimbaji Tumaini Msowoya ashinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Elimu

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Dr.Tumaini Msowoya ambaye pia ni mwandishi wa habari katika gazeti la Mwananchi amejinyakulia tuzo ya mwandishi bora wa habari za elimu kwa mwaka 2017 katika tuzo za Excellence In Journalism Awards Tanzania (EJATA) ambazo hufanyika kila mwaka.

Sambasamba na tuzo hiyo Dr. Tumaini amepatiwa scholarship(udhamini wa masomo) wenye thamani ya shilingi milioni mbili za kitanzania kutoka katika taasisi ya Haki Elimu ili aweze kujiendeleza katika taaluma yake.

Kupitia channel yako pendwa ya Gospo TV leo tumekuletea kwa ufupi jinsi tukio hilo lilivyofanyika.

Kwa niaba ya uongozi na timu nzima ya Gospo Media tunatoa pongozi zetu za dhati kwa mwimbaji Dr. Tumaini Msowoya kwa kushinda Tuzo hii, Mungu azidi kubariki kazi yake na huduma yake ya uimbaji.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top