Habari

Mwimbaji Shadrack Robert Kuzindua album yake ya Ashengai,Desemba 4 GloryLand Internal Church Arusha.Usikose.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania kutokea nyanda za kaskazini Shadrack Robert ambaye anatamba na vibao vyake kama vile Aksante, El shadai, Nijaze Roho, na sasa anatamba na video yake mpya inayoitwa Malaika anatarajia kuzindua album yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Ashengai.

Uzinduzi huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake utafanyika Desemba 4 katika kanisa la Gloryland International Church kuanzia saa tano kamili hadi saa saba mchana.

Akiongea na GospoMedia, Shadrack ameweka wazi lengo la uzinduzi huo ni kuiweka wakfu album hiyo yenye nyimbo nane, kuitangaza rasmi kwa umma na katika siku hiyo atawapa vionjo vya album yake ya pili.

Hii ni album yangu ya kwanza, ina nyimbo nane. Dhumuni kubwa la uzinduzi huu ni kuiweka wakfu ili iwe tayari kwa mauzo pia siku hiyo nitawaonjesha watu album yangu ya pili” alisema Shadrack.

Kwa wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani tujitokeze kwa wingi ili kumtia moyo mwana wa Mungu Shadrack Robert katika uzinduzi wa album yake mpya iliyobeba jina la ASHENGAI, Kumbuka ni Desemba 4 katika kanisa la GloryLand International Church kuanzia saa tano kamili asubuhi. Wote mnakaribishwa sana.

gospomedia.com tunakukaribisha pia kuitazama video mpya ya MALAIKA kutoka kwa mwimbaji Shadrack Robert ambapo pia unaweza kuupakua wimbo huu hapa chini kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kumpa sapoti mwimbaji Shadrack Robert na hakika utabarikiwa sana kwa ujumbe ulio katika wimbo huu na video hii. Karibu!!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Shadrack Robert kupitia
Simu/WhatsApp: +255767897260
Facebook: Shadrack Robert
Instagram: @shadrackroberts2
YouTube: Shadrack Robert
Email: thisisshadrack@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Onstage:Mwimbaji Lightness Vincent alivyoimba Live kwenye uzinduzi wa album yake ya Sitasumbuka Novemba 13,Miasha ya Ushindi Church.

Next post

Habari Picha za Tamasha la Mshindi wa Tatu wa GSS-2016 Rogate Kalengo Lililofanyika Novemba 13-2016.