Connect with us

Mwimbaji Ritha Komba Kuja na Video Mpya Mwezi Oktoba, ”Nitashinda”.

Habari

Mwimbaji Ritha Komba Kuja na Video Mpya Mwezi Oktoba, ”Nitashinda”.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania Ritha Komba ameweka wazi ujio wa video yake mpya iitwayo ”Nitashinda” anayotarajia kuiachia mwezi wa kumi ikiwa imeongozwa na Director Khalfan Khalmandro na wimbo ukiwa umetengenezwa na prodyuza Kingsong kutoka studio yake iitwayo Ritha’s Records.

Akiongea na mwanahabari wa gospomedia.com Ritha Komba amesema kuwa ujio wa video hii mpya itakwenda kuachilia baraka na nguvu ya matumaini kwenye nafsi za watu mbalimbali ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakishuka kiroho kutokana na kukosa matumaini ya kufanikiwa katika yale ambayo wanapigania hivyo ujio huu ni wa kuwaletea tumaini na nguvu ya kusonga mbele kwakuwa Yesu Kristo anafahamu shida na matatizo yao jambo wanalotakiwa kufanya ni wao tu kukubali kumkabidhi mizigo yao inayowatesa kama ni magonjwa, matatizo ya ndoa, Ajira, Uchumi kuyumba na mengine mengi na kupitia jina la Yesu watapata ushindi na kumtukuza Mungu katika kiwango cha juu sana.

Pamoja na hayo Ritha Komba ameomba watu kuendelea kumpa sapoti ili kuendelea kufanya kazi zake katika kiwango bora zaidi katika kuhakikisha Injili inawafikia watu wote ili ufalme wa Mungu uzidi kukua.

Katika Pozi: Mwimbaji Ritha Komba akionekana akiwa katika eneo analofanya video yake mpya.

kupitia blog yako pendwa tutaendelea kukuhabarisha kuhusu ujio huu ambao tutauweka hapa baada ya kuachiwa rasmi na naaamini utaachilia nguvu ya matumaini juu yako.

Kama bado hujatazama video yake ya Kivulini Karibu utazame na upakue wimbo huu na usiache kusubscribe channel yake ili uweze kupokea kazi zake anazoendelea kuziachia. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ritha Komba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Email: rithakomba@yahoo.com au synyoritha@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top