Habari

MWIMBAJI MWAMINI MUYERO KUZINDUA ALBUM YAKE YA NIMEPATA PUMZIKO TAREHE 23/10/2016,HUTAKIWI KUKOSA..

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Mwamini Muyero  anatarajia kuzindua album yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la NIMEPATA PUMZIKO jumapili ya tarehe 23/10/2016 katika kanisa la CAG Ubungo (kwa mchungaji Maboya) kuanzia saa nane kamili mchana na kuendelea.

Akiongea na GospoMedia.comMwamini Muyero amesema kuwa dhumuni kuu la uzinduzi huo ni kuiweka wakfu album yake iliyo katika mfumo wa DVD na kukusanyika pamoja na waimbaji wengine kumsifu Mungu pamoja.

Katika uzinduzi huo mwimbaji Mwamini Muyero atasindikiwa na waimbaji kama Ambwene MwasongweJessicah BMTheofrida GervasCatherine MkomaGideon Mhule , Grace MashaManesa SangaHoboke MpasileDorcas Lindu, Lenick JoachimKingdom ChoirProphetic Choir na CAG Praise Team.

Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kufika kwenye uzinduzi huo piga simu namba +255769 698909 na +255719 850559, Hakuna Kiingilio chochote, Wote mnakaribishwa!.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Paul Clement - Amenifanyia Amani

Next post

JOSHUA MAKONDEKO AWAJIA JUU CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI,NI BAADA YA KUTOONEKANA KWENYE MSIBA WA MKE WA JACKSON BENTY