Mwimbaji James Nyambega Atamani Kufanya Colabo na Witness Mbise. - Gospo Media
Connect with us

Mwimbaji James Nyambega Atamani Kufanya Colabo na Witness Mbise.

Uncategorized

Mwimbaji James Nyambega Atamani Kufanya Colabo na Witness Mbise.

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina James Nyambega ameeleza wazi kuwa ana ndoto ya kufanya kazi ya nyimbo za injili na mwimbaji mahiri Witness Mbise kwani amekuwa ndio mwimbaji anaye mvutia zaidi nchini.

Hayo ameyabainisha katika mahojiano yake ndani ya kipindi cha gospel cha Sua Fm, Nyambega alienda mbali zaidi na kusema kwamba anahitaji kufanya colabo na waimbaji wa kimataifa kwani kufanya hivyo kutakuwa ni kutangaza injili kimataifa zaidi.

Kwa upande wake Witness Mbise ameahidi kumpa ushirikiano mwimbaji huyo kama ataomba kufanya colabo na yeye.

Mwimbaji James kwasasa anatamba na wimbo wake mpya uitwao Nibariki Hivyo Hivyo ambapo kupitia wimbo huu mwimbaji James anatoa ushuhuda wa magumu aliyopitia na anayoendelea kupitia kabla na baada ya kumpokea Yesu Kristo na sasa ameamua kumlilia Mungu kupitia nyimbo hii juu ya kuomba kubarikiwa hivyo hivyo alivyo ili aweze kuwa huru na magumu na makwazo yanayomzuia kufika mafanikio yake kwa kuwa anaamini kupitia uwezo mkuu wa Mungu yeye atapona. Hakika ni wimbo wa kubariki na kuinua sana hasa kwa wewe uliyekata tamaa kutokana na magumu mbalimbali yanayokusumbua katika maisha yako.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha tena kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye kukubariki na kukuinua na hakika utakubarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji James Nyambega kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 655 315 428
Facebook: James Nyambega
Instagram: @jamesnyambega
Youtube: jamesnyambega@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Uncategorized

To Top