Habari

Mwimbaji Beatrice Muhone awashangaa wasiotaja Jina la Yesu Hadharani

Mwimbaji Mkongwe wa muziki wa injili hapa Tanzania Beatrice Muhone mwenye makazi yake Jijini Arusha ameshangazwa na watu wanaodai wameokoka lakini hawalitaji jina la Yesu Hadharani.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook mwimbaji huyo ameshangazwa na baadhi ya watu ambao huwa wanajitangaza kwa watu wameokoka na wengine wakiwa ni waimbaji wa muziki huo lakini katika  nyimbo zao hawalitaji jina la Yesu kuanzia wimbo wa kwanza mpaka wa Mwisho.

Sehemu ya ujumbe wake ulisomeka kwamba”Ila swali moja likufikirishe inakuwaje umeokoka ila kumtaja Yesu hadharani kwako ni shida, Kwanini?“Alihoji Mwimbaji huyo.

Beatrice Muhone ni miongoni mwa waimbaji ambao walitamba sana miaka mingi ya nyuma na  nyimbo kama Habari Njema, Ingoje Ahadi na nyingine ambazo mpaka sasa zinaishi  nyimbo zake.

Mawasiliano ya Beatrice Muhone
Facebook: Beatrice Muhone.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Rose O. Mollel Chipe - Hakuna Kama Yesu

Next post

Director Einxer,Pyuza,Kilonzo kukutana ndani ya Tamasha la The Big Praise Concert Dar June 18