Connect with us

Mwimbaji Anna Mapessa Kuachia Wimbo Wake Mpya Tarehe 15 Septemba 2017

Habari

Mwimbaji Anna Mapessa Kuachia Wimbo Wake Mpya Tarehe 15 Septemba 2017

Mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili kutoka kwa jijini Dar es salaam Anna Mapessa yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya uitwao ”Unaweza” ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kuachia kwa mwaka huu 2017 ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Makini Studios chini ya mikono ya prodyuza Enock Jonas.

Akiongea na timu ya wanahabari wa gospomedia mwimbaji Anna Mapessa amesema kuwa ujio wake huu mpya ni wa kusifu utukufu wa Mungu na kuwapa tumaini jipya wale wote ambao wapo katika mahangaiko mbalimbali ya kiroho na kimwili na kuwakumbusha juu ya nguvu za Mungu juu yetu kama tukiamini na kumkabidhi Bwana wetu Yesu Kristo maisha yetu naye atafanya kwa upendo halisi katika kutuokoa na kutuponya nafsi zetu, Hivyo amewaomba wadau na mashabiki wote wa muziki wa Injili kumpokea na kumtia moyo katika safari yake hii aliyoianza ya kulitangaza neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Anna Mapessa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 658 489 575
Facebook: Anna Mapessa
Instagram: @annamahela
Twitter: @annamapessa
Youtube: Anna Mapessa

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top