Habari

Mwanamke akamatwa kwa kujaribu kuieneza Injili kwa Raisi wa China

Mwanamke mmoja raia wa nchini China amekamatwa na maafisa wa usalama wa umma na kuwekwa kizuizini baada ya kujaribu kuieneza injili kwa Raisi wa nchi hiyo Xi Jinping.
Taasisi ya waangalizi wa mtazamo wa mateso ya wakristo nchini china(Persecution watchdog China Aid) imesema kuwa Machi 15, 2018 Zhou Jinxia, ​​Mwanamke mkristo ambaye alisafiri kwenda Beijing kutoka Dalian, aliwasili kwenye mlango wa mbele wa bustani ya zamani ya ikulu Zhongnanhai, akiwa na bango lenye ishara ya msalaba na maneno yanayosomeka, “Mungu anapenda watu wa ulimwengu na huu ni wito kwa Xi Jinping. ”

Taasisi hiyo imesema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuufikisha ujumbe wake kwa Raisi Xi wakati mkutano wa chama cha   The National People’s Congress (NPC) na chama cha The Chinese People’s Political Consultative Conference (CPPCC).

Taasisi ya waangalizi wa mateso ya wakristo duniani ( Persecution watchdog Open Doors USA) imesema kuwa China imechukua nafasi ya 43 katika orodha ya nchi 50 duniani ambapo Wakristo wanakabiliwa na mateso zaidi.

Chanzo kikuu cha mateso hayo kikiwa ni sera na mifumo ya serikali za Kikomunisti(Ujamaa), Open Doors imesema.

“Wakristo, husuani waishio nchini China wanakabiliwa na mamlaka za kiserikali, kwa kuwa wao ndio nguvu kubwa zaidi ya kijamii nchini China,” imesema taarifa hiyo.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Evelyn Wanjiru - Jehovah Elohim | Its Amazing

Next post

Papa Francis awaasa vijana kutokukaa kimya, kusali na kuomba