Habari

Mwanafizikia Stephene Hawking kuhifadhiwa katika eneo la kanisa

Na Mwandishi wetu,

Nchini Uingereza taarifa imetolewa kuwa majivu ya mwanafizikia Stephene Hawking yatahifadhiwa katika eneo la Kanisa na jumba la makumbusho Westminster Abbey mjini London karibu kabisa na mabaki ya baadhi ya wanasayansi nguli waingereza, Isaac Newton na Charles Darwin.

Mkuu wa mji wa Westminster, John Hall anasema sayansi na dini vinatakiwa kufanya kazi pamoja kutafuta majibu ya maswali mazito ya siri ya maisha na Ulimwengu.

Kabla ya kufariki, Stephene Hawking alisema Sayansi haiwezi kuthibitisha kuwa Mungu hayupo, lakini inamfanya kuwa si wa muhimu.

Katika andiko lake la mwisho, Stephene Hawking alieleza juu ya milipiko na migongano isiyokwisha ya sayari huko angani kiasi cha kila mgongano kutengeneza Ulimwengu wake.

Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka. Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama ‘Black Hole’.

Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: “Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha.”

“Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi.”

Mambo muhimu kuhusu maisha ya Stephen Hawking

  • Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England
  • Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge
  • Kufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.
  • Alieleza nadharia yake kwamba ‘black hole’ kutoa “Miali ya Hawking” mwaka 1974
  • Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.
  • Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo

Hawkings aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa mfumo wa neva akiwa chuo kikuu

Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Ejiro Melkam – Deserved

Next post

Wakristo wa kivietinamu washambuliwa, wakilazimishwa kukataa ukristo