Habari

MWANA GOSPEL HIP HOP WA MAREKANI, LECRAE ATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA

Mwanamuziki maarufu wa Gospel Hip Hop nchini Marekani Lecrae Moore ametunukiwa udaktari wa hesima katika mambo yanayohusu muziki na chuo cha Canada Christian College akiwa kwenye ziara yake ya vyuoni aliyoipa jina la Higher Learning Tour.

Lecrae amekuwa mtu mwenye umri mdogo kutunukiwa heshima hiyo kutoka kwenye chuo hicho ambacho kimewahi kuwatunuku heshima hiyo watu kama Hon. Jim Flaherty, lieutenant-governor David Onley, Rev. Franklin Graham.

GospoMedia tunampongeza Lecrae ambaye kwa sasa atakuwa akiitwa Dr.Lecrae kwa kutunukiwa heshima hiyo ambayo imetokana na mchango wake kwenye kushawishi jamii kushiriki kwenye mambo chanya, na ifanyike changamoto kwa waimbaji wengine pia.

Chanzo: Rapzilla

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
YESU OKOA MITAA
Previous post

YESU OKOA MITAA KUACHIA NGOMA MPYA KESHO, JINA LAKE HILI HAPA.

Next post

DOWNLOD MUSIC AUDIO: ALFREDY FUNDA - USIKATE TAMAA