Habari

Mwana Gospel Hip Hop Novic BCVM Aweka Wazi Mipango Ya Huduma Yake Kwa Mwaka 2017.

Mwana Gospel Hip Hop kutoka kwenye lebel ya Wa Nuru Novic Daniel maarufu kama BCVM ameweka wazi mipango yake ya mwaka 2017.

Akizungumza kwenye Gospel News ya kipindi cha Praise Time kinachorusha na kituo cha Radio cha Habari Maalum Fm Arusha Novic amesema anamshukuru Mungu kuwa mwaka 2016 ulikuwa mwaka mzuri kwake kwasababu alifanikiwa kuachia Gospel Rap Mix Tape yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo nane.

Novic amesema amejipanga vizuri kwa mwaka 2017 na watu wategemee mambo mazuri toka kwake.

“mwaka huu wa 2017 kwangu utakuwa mwaka wa tofauti na watu wategemee kumuona Novic kwenye colabo na wasanii wengine wa nyimbo za injili”

Ameeleza kuwa tayari ameshafanya kazi ya kushirikiana na wasanii kutoka Nairobi Kenya, wimbo unaitwa ukweli na uko youtube kupitia link hii https://youtu.be/cv9mylfYxmA  unaweza utazama wakati wowote.

Novic akiwa jukwaani

Novic ameeleza kuwa amefanya kazi na waimbaji wanaofanya Gospel Hip Hop lakini nyingine amefanya na waimbaji wanaoimba kawaida na kazi zote hizo zitaachiwa mwaka huu.

Pamoja na hayo Novic ameweka wazi kuwa ataanza kushoot video za nyimbo zake kwahiyo watu wategemee pia kuona Video nzuri toka kwake.

Ameweka wazi kuwa ni mapema sana kuzungumza kuhusiana na kufanya Mix Tape ya pili kwa mwaka huu ila watu wategemee mambo mazuri toka kwake mwaka huu 2017.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Janet Otieno-Bisha

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Faith Mission Vijana Choir Chato-Nitalitangaza