Connect with us

Music Video: Phidelis Kindole – Hakuna Kama Wewe

Muziki

Music Video: Phidelis Kindole – Hakuna Kama Wewe

Shalom mwana wa Mungu leo kupitia blog yako pendwa nimekusogezea video iitwayo ”Hakuna Kama Wewe” kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Phidelis Kindole, video ikiwa imeongozwa na director Bancello Tieono kutoka studio za Experience Picturez na audio ikiwa imetayaarishwa ndani ya studio ya Mbogo Production chini ya mikono ya prodyuza Itika.

Phidelis Kindole ni kiongozi wa kundi la waimbaji wa muziki wa Injili liitwalo East Africa Gospel Musician’s ambalo liawaunganisha waimbaji kutoka Tanzania na Kenya na limekuwa likijihusisha kuandaa matamasha katika nchi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika.

Hakuna kama wewe ni moja ya video inayopatikana kwenye albamu yake ya pili iitwayi Sifa na Utukufu ikiwa inapatikana kwenye mfumo wa video DVD  na Audio CD na tayari ipo sokoni kwasasa ikiwa inapatikana kwenye maduka mbalimbali ya wasambazaji nchi nzima.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Phidelis Ndole Kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 713 594 224, +255 678 340 925
Facebook: Phidelis Ndole
Youtube: Phidelis Ndole

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top