Connect with us

Music Video | Music Audio: Sakina Naftali – Yatakwisha

Muziki

Music Video | Music Audio: Sakina Naftali – Yatakwisha

Shalom mwana wa Mungu leo kupitia blog yako pendwa nimekuletea video na wimbo wenye kubariki na kuinua sana moyo uitwao Yatakwisha kutoka kwa mwimbaji mahiri na mwenye sauti ya kipekee katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Sakina Naftali kutoka moshi, kilimanjaro. Video hii nzuri imeongozwa na director anayefahamika kwa jina la Director Sam Tz na wimbo ukiwa umetayaarishwa na prodyuza mkali anayefahamika kwa jina Alonem.

Mtumishi wa Mungu Sakina Naftali kupitia wimbo huu ametumika kuimba wimbo huu kwa lengo la kutukumbusha na kututia moyo kupitia Neno la Mungu ambalo ameliweka katika muziki wa Injili na hakika huu ni moja kati ya wimbo ambao utakuinua na kukupa nguvu mpya ya matumaini katika yale ambayo unayapitia hata kama ni magumu kiasi gani bado Bwana Yesu yupo kwa ajili yetu kutupigania na kuhakikisha tunakuwa furaha na amani kwa utukufu wa Mungu.

”Katika magumu, mapito na hali zozote ambazo tunapitia kama wanadamu, tuwe na imani kwamba iposiku yote Yatakwisha. kila jaribu linamlango” – Sakina Naftali

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nzuri na kupakua wimbo huu wenye kubariki mno na hakika utabarikiwa na kuinuliwa kwa zaidi unavyoendelea kutazama na kusikiliza kila siku. Karibu sana!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Sakina Naftali kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 654 114 947
Facebook: Sakina Naftali Stanley
Instagram: @sakinanaftali
Youtube: Sakina Naftali

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top