Video

Music Video | Music Audio: Same OG – Power

Rapa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Same OG ameachia wimbo uitwao Power ukiwa ni wimbo unaozungumzia moyo wa Mtu wa kawaida ambaye ana ndoto na anatamani kumfuata Yesu ili awe na nguvu ya kumshinda shetani lakini anahisi kama bado haiwezekani, lakini kupitia wimbo huu rapa Same OG anatukumbusha kuwa Mungu yu pamoja nasi pale hata kabla ya kuumbwa kwetu alishatujua na nini kusudi letu katika dunia hii.

Wimbo huu aliuachia siku ambayo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa Alhamisi ya Novemba 2, 2017 na aliachia wimbo huu ikiwa ni zawadi yake katika kuwahamasisha vijana katika kumtegemea Mungu ili waweze kushinda vita na vifungo vya shetani.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Karibu upate Power!.

Download Audio

Social Media
Twitter:@its_sameog Instagram: @its_sameog Youtube: OfficialSameOG
www.sameog.com/music

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Music Audio: Lukrensia Mlelwa - Karibu Yesu

Next post

Audio Music: Pompi - Kapena