Videos

Music Video | Download Music Audio: Noah Sinene – Pokea

Shalom mwana wa Mungu!! leo kwa utukufu wa Mungu nakukaribisha kutazama video iitwayo Pokea kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina Noah Sinene akipatikana wilayani Makete mkoani Njombe. Video hii imeongozwa na director anayefahamika kwa jina la Mr.Shine kutoka studio za Shine Star entertainment na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Vision Records iliyopo makete.

Video hii inapatikana kwenye albamu yake mpya iitwayo ”Nakutegemea” ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane na inapatikana kwenye mfumo video DVD.

Moja ya mambo ambayo Mungu huyapima kwa wanadamu ni kwa jinsi gani wanavyomtolea shukurani ikiwa ni pamoja na Sadaka safi yenye kumpendeza yeye na hapo ndipo upendo wake hujidhirihirisha na kushusha baraka takatifu juu ya maisha yetu. Kupitia wimbo huu wa Pokea mwimbaji Noah Sinene anatukumbusha jambo jema linalohusu umuhimu wa kumtolea Mungu sadaka hata kwa kile kidogo ambacho unacho kitoe kwa moyo wako wote bila manung’uniko na Mungu atakwenda kukibariki katika kiwango cha hali ya juu sana kufanya maisha yako kuwa ya kiwango kingine.

Kwa moyo wa unyenyekevu nakukaribisha kuitzama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi, huduma ya mialiko wasiliana na kupata nakala ya albamu hii wasiliana na mwimbaji Noah Sinene kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 758 860 857 au +255 785 734 117
Facebook: Noah Sinene
Instagram: @noahsinene
Youtube: Noah Sinene
Email: noahdenissinene@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio Music: Jive Angels Feat Buchi - God is Good

Next post

Download Official Music Audio: Estherlyn - Emmanuel