Videos

Music Video | Audio: Neema Mudosa – Hawawezi

Kutoka kwa mtumishi wa Mungu Neema Mudoa leo kwa mara nyingine anakukaribisha kuitazama video ya wimbo wake uitwao Hawawezi iliyoongozwa na Director Joowzey kutoka studio za Joh Films na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Mpo Africa chini ya mikono ya Goodluck Gozbert.

Hawawezi ni wimbo mzuri uliobeba ujumbe wenye kusudi la kukupa nguvu ya kuamini katika ushindi ndani ya Yesu, tunajua kuwa hali ya dunia ya leo imejaa misongo na majaribu ya kila aina ambayo mengi yanasabishwa na binadamu wenyewe kiasi ambacho unarudi nyuma na kumwacha Mungu lakini leo kupitia wimbo huu Neema Mudosa anakutia moyo na kukuhimiza kukiri ushindi juu ya watu wanaotaka uanguke na kuwa mbali na Mungu..

Tambua kuwa upendo na mipango ya Mungu juu ya maisha yako haiwezi kuzuiwa wala kubadilishwa na binadamu yoyote kwakuwa yeye pekee ndiye mwenye mamlaka juu yetu na vyote vilivyopo duniani na mbinguni.. hivyo amini Hawawezi kubadilisha mpango wa Mungu, kusudi la Mungu juu yako.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani utaufurahia, utakubariki na kukuinua. Karibu!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Neema Mudosa kupitia
Simu/WhatsApp: +255654 782 575
Facebook: Neema Guillaine Mudosa
Instagram: @neemamudosa

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Audio: Ashley Nassary - Ni Neema

Next post

Music Audio: Abraham K - Stronger