Connect with us

Music Audio: Rhoda Itenya – Ni Neema

Muziki

Music Audio: Rhoda Itenya – Ni Neema

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu! kwa utukufu wa Mungu leo tena nimekuletea wimbo uitwao ”Ni Neema” kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la ”Rhoda Itenya” au unaweza kumwita Riama Itenya, wimbo ukiwa umefanyika ndani ya studio za Exodus chini ya mikono ya Prodyuza Gilbert Noah.

”Pale ambapo unapata nafasi ya kumshukuru Mungu basi na ufanye hivyo ili aweze kukupa baraka zaidi kupitia jina la Yesu Kristo kwakuwa Ni Neema hata kwa wewew kuwa hapo ulipo” – Rhoda Itenya

Huu ni wimbo mwingine uliojaa maneno ya matumaini na habari njema kutoka kwa mtumishi wa Mungu Rhoda Itenya ambaye kwa hakika anazidi kuwa baraka kwa watu wengi kupitia huduma yake ya uimbaji hasa baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza uitwao ”Funguka” na sasa amekuja na wimbo huu wa sifa na wa kumshukuru Mungu kwa yale ambayo Mungu amemtendea mpaka hapo alipofika na huu ni ukumbusho hata kwetu sisi wana Mungu kuwa Ni Neema na huruma yake pekee ndio imetufikisha hapa tulipo hivyo hupaswi kujiiunua na kuwadharau wengine kwakuwa Mungu ndiye mkuu wa vitu vyote.

Hakika ni wimbo mwingine mzuri uliojaa maneno ya faraja na mafundisho kwako wewe mwana wa Mungu, kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana siku ya leo.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Rhoda Itenya Kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 360 866
Facebook: Riama Itenya
Instagram: @riamaitenya

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top