Music Audio: Gold Anuli Feat. Dare Justified – Babaa - Gospo Media
Connect with us

Music Audio: Gold Anuli Feat. Dare Justified – Babaa

Audio

Music Audio: Gold Anuli Feat. Dare Justified – Babaa

Kutoka nchini Nigeria leo nimekusogezea wimbo uitwao Babaa kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Gold Anuli akiwa amemshirikisha mwimbaji mahiri anayefahamika kwa jina la Dare Justified, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za T Groopz Music chini ya mikono ya prodyuza Oweck.

Akiongea na mtandao gospelify mwimbaji Gold Anuli alisema:-

“Babaa ni wimbo wa ujio wangu mpya baada ya kuachia wimbo uitwao KULIENU miaka mitatu iliyopita, na nakiri kuwa ukamilifu wa kazi hii nzuri si kwa akili zangu bali ni Mungu. Ingawa mimi ni mtunzi mzuri wa nyimbo lakini siwezi kuchukua nafasi hii kusema kwamba ndiye niliyeandika wimbo huu naamini ni Mungu tu.

Kupitia hili ninapenda kutoa ushuhuda wa wimbo huu kwamba kuna siku niliamka asubuhi moja na kuanza kusikia  aya za muziki kwenye masikio yangu yaani nilikuwa nasikia sauti za muziki na aya za wimbo wote. Niliandika tu yale niliyoyasikia kwenye simu kupitia sauti yangu niliyoamka nayo usingizini na hakika Mungu alifanya jambo kuu sana katika kufanikisha kazi hii ambayo nimemshirikisha Dare Justified ambaye niliamini kuwa ataweza kufanya wimbo huu wa sifa kuwa bora zaidi na wenye kumpendeza Mungu.

Ni heshima yangu mbele za Mungu kuwa wimbo huu utakwenda kuweka neno lenye kupendeza kwenye masikio ya watu wengi zaidi na hakika  Mungu atatukuzwa daima kupitia wimbo huu.” – Alimaliza Gold Anuli

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Karibu!!

 

Download Audio

Gold Anuli Social Media
Facebook:Gold Anuli De Ambasadore Fans Page
Instagram:@goldanulivoicecoach
Twitter: @goldanuli

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Audio

To Top