Connect with us

Music Audio: Damichromes – Great is your Love

Muziki

Music Audio: Damichromes – Great is your Love

Kutoka nchini nigeria leo nimekuwekea wimbo uitwao ”Great is Your Love” kutoka kwa mwimbaji anayefahamika kwa jina la DamiChromes, wimbo ukiwa umetaayarishwa na prodyuza FadaBen akiwa ni mtumishi pekee anayewasaidia waimbaji wadogo katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini humo kufikia ndoto zao.

DamiChromes ni kijana aliyebarikiwa na vipaji mbalimbali ikiwemo uimbaji na kuongoza nyimbo za sifa, uandishi wa nyimbo, upigaji wa vyombo vya muziki, na vipaji vingine vingi vinavyohusiana na muziki.

Great is Your Love ”(Upendo wako ni mkubwa)”ni wimbo wa kwanza kuachia ukiwa na unaelezea na kudhihirisha shauku yake ya kumtukuza Mungu kwa namna ya kipekee kupitia muziki huu ulio katika mtindo wa Pop na kuwakumbusha watu mambo ya zamani hasa miaka ya 80 na 90, na kuwavutia zaidi vijana na wazee.

Wimbo huu unapanua ukuu wa upendo wa Mungu ambaye alimtuma Yesu Kristo kwetu na kukubali kuteswa na kufa msalabani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote ulimwenguni.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu kwa mara ya kwanza nikiamini utaweza kuufurahia na kubarikiwa.

 

Download Audio

DamiChromes Social Media
Facebook:Damichromemusic
Instagram:@damichromesm

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
Advertisement
You may also like...
Advertisement

TRENDING

To Top