Habari

Muimbaji Tasha Cobbs Arekodi Wimbo na Nicki Minaj Kwenye Album Yake Mpya.

 

Kutoka nchini marekani muimbaji maarufu wa nyimbo Injili na mshindi wa Tuzo ya Grammy, Tasha Cobbs-Leonard, amemshirikisha mwanamuziki na rapa maarufu nchini humo anayefahamika kwa jina la Nicki Minaj kwenye albamu yake mpya inayotarajia kuiachia hivi karibuni ikiwa imebeba jina la ‘Heart. Passion. Pursuit’.

Katika album hiyo Tasha Cobbs amemshirikisha Nick Minaj kwenye wimbo uitwao “I’am Getting Ready” ukiwa ni wimbo wa nane katika mtiririko wa nyimbo kumi zinazopatikana kwenye album hiyo inatarajiwa kuachiwa tarehe 25 Agosti 2017 ambapo kwasasa watu wameanza kuinunua kwa kuweka oda kupitia mfumo wa manunuzi ya album hiyo.

Wasanii wengine walioshiriki kwenye albamu hii ni pamoja na Anna Golden, William Murphy, Jimi Cravity, na Kierra Sheard.

Miaka miwili iliyopita, Nicki Minaj alitazama tukio la sherehe za muziki wa injili la BET kupitia televisheni 2014 , ambapo alimuona Tasha Cobbs-Leonard na Jonathan McReynolds wakitumbuiza pamoja na kuanzia hapo Nick Minaj akawa amevutiwa na muziki wa Injili na waimbaji wa muziki huo.

Baadaye Minaj aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter juu ya kutamani kushirikiana na Tasha Cobbs, “Utakapomaliza kurekodi albamu, uje kwenye studio yangu ili niweze kuweka mistari 16 kwenye moja ya nyimbo hizo! Aliandika Nick Minaj na matarajio yake yakawa kweli.

Mara baada uvumi wa habari kuenea juu ya Nicki Minaj kushiriki kwenye albamu hiyo, Tasha Cobbs aliamua kuthibitisha kwa kuandika ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusiana na ushiriki wa Nick Minaji kwenye album hiyo hasa kwa watu ambao walikuwa hawaamini na kupinga vikali juu ya ushirikiano huo.

Kwa upande mwingine Tasha Cobbs amepata upinzani mkali kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili na mashabiki wake juu ya kumshirikisha Nicki Minaji kwenye album yake hiyo inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni, japo yeye pia amajitetea na kusema kuwa watu wasiwatenge waimbaji wa kidunia kwa kuwa Mungu ana makusudi juu kushughulikia historia zao, hivyo kumshirikisha Nicki Minaj ni moja ya nafasi ya kuleta mabadiliko ya kiroho juu ya maisha yake na ya watu wengine. Warumi 14: 1

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: T.S Itopa Feat Johnny K. Palmer - Unrestrained

Next post

Download Music Audio: Geo Feat Josh - On My Nerves