Habari za Muziki

Muimbaji Shawn Jones aanguka na kufa wakati akihudumu madhabahuni.

Na Mwandishi Wetu, Marekani;

Shawn Jones, mwimbaji wa nyimbo za injili na mchungaji kiongozi wa Kanisa la The New Thing Empowerment Church lililopo mjini Auburn, Alabama, alianguka na kufa wakati akihudumu na bendi yake iitwayo The Believers hivi karibuni katika ukumbi wa Pensacola mjini Florida, Marehemu Shawn Jones amefariki akiwa na umri wa miaka 32.

Kanisa na wafuasi wa Mchungaji Jones watafanya Tamasha maalumu ambalo limebatizwa jina la The Shawn Jones Legacy Concert katika kumuenzi na kuwaunganisha watu pamoja katika kufanya maombi na kutoa rambirambi zao za pole kwa ndugu, familia na kanisa la Shawn Jones, ambapo siku ya jumanne asubuhi watu wote kwa pamoja watajumuika kuuaga mwili wa marehemu na kutoa salamu za mwisho katika kanisa la Pilgrim Rest Baptist Church.

Kupitia mtandao wa The Christian Post ulisema ”muda mfupi baada ya Jones kuanza kuimba wimbo uitwao  “Worthy Is He,” aliondoka ghafla kwenye macho ya watazamaji katika hali ya kushangaza.

Woodson alikumbuka bendi hiyo ilikuwa imekamilisha kuimba wimbo wao wa kwanza na kuanza kuimba wimbo wa “Worthy Is He,” Watazamaji walisimama, huku wakipiga makofi na kuimba pamoja na ghfla walimwona Shawn Jones akianza kupata shida.

“Nadhani kijana huyu alipata joto, akachukua maji na kunywa maji zaidi kwa mara ya pili, akaketi na kusema maneno kadhaa na kufa hapohapo,” Woodson aliuambia mtandao wa The Christian Post.

“Kila mtu alishtuka na nafikiri kila mtu alifanya yale waliyoona yalikuwa sawa katika kujaribu kuokoa maisha ya Shwan Jones mpaka madaktari wa EMT(Emergence Medical Technician) walipofika hapa, ilikuwa ni mshtuko mkubwa kwa sababu yeye alikuwa bado ni kijana,” aliendelea.

Mpaka sasa sababu ya kifo cha Jones bado haijatangazwa. Hata hivyo, mmoja wa waimbaji wa Bendi ya The Echoaires of Memphis, aitwaye Tenn, ambaye pia alikuwa amepangwa kuhudumu katika tukio hilo, alisema Jones amekufa kwa shambulio la moyo.

Tamasha maalum la kumuenzi Shawn Jones litafanyika kwenye Kanisa la Pilgrim Rest Baptist huko mjini Montgomery, Alabama leo Jumatatu, Novemba 27, Tamasha hilo litakuwa mubashara kwenye tovuti ya shawnjoneslegacy.com

Ibada maalumu ya kumuaga ya Shawan Jones itafanyika Jumanne, Novemba 28 saa 10:30 asubuhi Ibada hii pia itakuwa mubashara kwenye tovuti ya shawnjoneslegacy.com.

Huu ndio wimbo wa kwanza alioutumia kuhudumu katika ukumbi wa Pensacola, Florida Jumamosi ya 11/18/2017 kabla ya mauti kumfika.

Mungu amuweke mahali pema Mchungaji Shawn Jones.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Music Audio: Walter Chilambo - Kuna Jambo

Next post

Audio Music: EAGT Buzuruga - Tufurahi